Je, Tumesulubiwa Pamoja na Kristo? [Are We Crucified With Christ?]

Wengi wetu hatujaelewa kikamilifu jinsi adhabu ya Kirumi ya kupigwa mijeledi na kusulubiwa ilivyokuwa njia ya kutisha sana na ya aibu ya kuuawa.

Ni ajabu kwamba Yesu aliweza hata kufika Golgotha ukizingatia mateso ya kupigwa mijeledi aliyopokea. Adhabu ya Wayahudi ya mapigo 39 – au michubuko – kwenye ngozi ilikuwa na kikomo kwa sababu kulikuwa na hatari ya kumuua mtu anayeadhibiwa.

Hata hivyo Warumi — waliokuwa wakijulikana kwa ukatili wao na tamaa yao ya kuona damu — walitengeneza kwa makusudi mijeledi yenye kamba za ngozi zilizofungwa mafundo na vipande vya mifupa au chuma ili kuhakikisha kwamba vipande vya nyama vinachomoka kwa kila pigo la mjeledi. Nao hawakuwa na kikomo cha sheria au desturi za Kiyahudi cha mapigo 39 tu.

Mwonekano wa kimwili wa Yesu lazima ulikuwa umeharibika sana kiasi kwamba karibu usingetambulika kufikia alipofika mahali pa kusulubiwa.

Isaya 52:14 (NCV)
14 Kama vile wengi walivyokustaajabia, uso wake ulikuwa umeharibiwa sana Zaidi ya mtu ye yote, na umbo lake Zaidi ya wanadamu.

(NLT) 14 Wengi walishangaa walipomwona—amepigwa na kujaa damu, akiwa ameharibika sana kiasi kwamba ilikuwa vigumu kutambua kama alikuwa mtu.

Zaburi 22:14–17 (NLT)
14 Nimemwagika kama maji, Mifupa yangu yote imeteguka. Moyo wangu umekuwa kama nta, Na kuyeyuka ndani ya mtima wangu.
15 Nguvu zangu zimekauka kama gae, Ulimi wangu waambatana na taya zangu; Unaniweka katika mavumbi ya mauti.
16 Kwa maana mbwa wamenizunguka; Kusanyiko la waovu wamenisonga; Wamenizuia mikono na miguu.
17 Naweza kuihesabu mifupa yangu yote; Wao wamenitazama na kunikodolea macho.

Haya ndiyo Kristo aliyopitia miaka 1992 iliyopita.

Maandiko yanasema tulinunuliwa “kwa gharama.” Hakuna gharama kubwa zaidi ambayo ingeweza kulipwa na Baba pamoja na Mwana. Ni aina gani ya upendo tunaonyeshwa kupitia tendo hili la hiari?

Sisi pia tuna wajibu kwa Kristo badala yake. Ni lazima tuonyeshe heshima yetu kwa kile alichotufanyia.

Tunafanyaje? Paulo alifanyaje?

Wagalatia 2:20 (NKJV)
20 Nimesulubiwa pamoja na Kristo; lakini ni hai; wala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani yangu; na uhai nilio naoi sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa Mungu, ambaye alinipenda, akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu.

(NCV) 20 Niliuawa msalabani pamoja na Kristo, nami siishi tena—ni Kristo anayeishi ndani yangu. Bado ninaishi katika mwili huu, lakini ninaishi kwa imani katika Mwana wa Mungu aliyenipenda na kujitoa mwenyewe kuniokoa.

Ni lazima tuonyeshe heshima na adabu yetu kwa Shujaa wetu aliyeanguka kwa kujisulubisha pamoja naye kama Paulo alivyofanya. Kuna mambo matatu muhimu kuhusu hili:

1. Kuwa na mtazamo wa kiheshima

2 Samweli 11:6–11 (NLT)
6 Ndipo Daudi akapeleka kwa Yoabu, akisema, “Unipelekee Uria, Mhiti.” Naye Yoabu akampeleka Uria kwa Daudi.
7 Uria alipomwendea Daudi, Daudi alimwuliza habari za Yoabu, na habari za watu, na habari za vita.
8 Daudi akamwambia Uria, Haya, “shuka nyumbani kwako, ukanawe miguu yako.” Basi Uria akatoka katika nyumba ya mfalme, na tunu ya vyakula ikamfuata, iliyotoka kwa mfalme.
9 Lakini Uria akalala mlangoni pa nyumba ya mfalme, pamoja na watumishi wote wa bwana wake, wala hakushuka nyumbani kwake.
10 Watu walipomwambia Daudi ya kwamba, Uria hakushuka nyumbani kwake, Daudi akamwambia Uria, Je! Hukutoka safarini? Mbona hukushuka nyumbani kwako?
11 Naye Uria akamwambia Daudi, Sanduku, na Israeli, na Yuda, wanakaa vibandani; na bwana wangu Yoabu, na watumishi wa bwana wangu, wamepiga kambi waziwazi uwandani; nami niende nyumbani kwangu, kulan a kunywa, na kulala na mke wangu?. Uishivyo, na kama roho yako iishivyo, mimi sitafanya jambo hili.”

Uria alikuwa na mtazamo wa heshima kubwa sana kwa wenzake askari. Kwa mkuu wake Yoabu. Na pia alimjumuisha Mungu kwa kumtaja Sanduku la Agano. Alijinyima mwenyewe kwa heshima yao.

Ni lazima tupokee mtazamo wa Uria.

2. Kuwa tayari kuteseka

TUTATESWA. Kuacha kutenda dhambi kunaleta mateso!

Warumi 8:16–18 (NKJV)
16 Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu;
17 na kama watoto, basi, tu warithi—warithi wa Mungu, warithio pamoja na Kristo; naam, tukiteseka pamoja naye ili tupate na kutukuzwa pamoja naye.
18 Kwa maana nayahesabu mateso ya wakati huu wa sasa kuwa si kitu kama utukufu ule utakaofunuliwa kwetu.

1 Petro 4:1 (NLT)
1 Basi kwa kuwa Kristo aliteswa katika mwili wake, ninyi nanyi jivikeni silaha ya nia ile ile; Kwa maana yeye aliyeteswa katika mwili ameachana na dhambi.

Waebrania 12:1–4 (NLT)
1 Basi na sisi pia, kwa kuwa tunazungukwa na wingu kubwa la mashahidi namna hii, na tuweke kando kila mzigo mzito, na dhambi ile ituzingayo kwa upesi; na tupige mbio kwa saburi katika yale mashindano yaliyowekwa mbele yetu.
2 Tukimtazama Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu; ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake aliustahimili msalaba na kuidharau aibu, naye ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu.
3 Maana mtafakarini sana yeye aliyestahimili mapingamizi makuu namna hii ya watendao dhambi juu ya nafsi zao, msije mkachoka, mkizimia mioyoni mwenu..
4 Hamjafanya vita hata kumwagika damu, mkishindana na dhambi.

Je, tunaona kwamba kwa kulinganisha, kusulubiwa kwetu si kitu ukilinganisha na kusulubiwa kwa Kristo?

Tuonyeshe heshima yetu kwa kuvumilia mateso ya kuacha dhambi. Cho chote kile.

3. Kuwa na mtazamo wa vita

Paulo anaelezea jambo hili kwa ustadi mkubwa katika barua yake kwa Kanisa la Efeso.

Waefeso 6:10–18 (NLT)

10 Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake.

11 Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani.

12 Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.

13 Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.

14 Basi simameni, hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani,

15 na kufungiwa miguu utayari tupatao kwa Injili ya amani;

16 zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu.

17 Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu;

18 kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote.

Ni vita vya kudumu, na lazima tuwe tayari kwa jukumu hilo. Tukumbuke:

KWELI MBILI MUHIMU

(1) Vita vyako daima vina SABABU.
(2) Vita
vyako daima vina MUDA wake.

Tusisahau kamwe jambo hili.

Niliwahi kufundisha mpira wa kikapu kwa vijana kwa miaka 13.

Mazoezi yalikuwa magumu. Niliwafanya wawe katika hali nzuri ya kucheza kwa kuwafanya wavumilie maumivu. Watoto walifundishwa kwamba kuungua kwa ngozi sakafuni baada ya kujitupa kuokoa mpira ilikuwa “ishara ya heshima.”

Kazi yangu kama kocha haikuwa tu kuwafundisha misingi ya kitaalamu ya mchezo wa mpira wa kikapu.

Kazi yangu ilikuwa kuwafanya wachezaji wangu wawe tayari kucheza—tayari kutoa juhudi zao zote. Nilipaswa kuwahamasisha watake kushinda, na “kuacha kila kitu uwanjani.”

Basi na tujihami kwa mtazamo wa Uria. Na tujiandae kwa mateso. Na tupigane vita vya kishujaa dhidi ya dhambi, tukitumia silaha za vita tulizopewa na Mungu kama Paulo alivyoelezea.

Na tuwe na shauku ya kuingia vitani dhidi ya Ibilisi. Na tuwe tayari kuteseka na kupata alama za heshima. Na tuache kila kitu uwanjani.

Na tuhakikishe kwamba tunajisulubisha sisi wenyewe kwa heshima ya yale yote Kristo aliyopitia kwa ajili yetu.